Psalms 18:8-11

8 aMoshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake.
9 bAkazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
10 cAlipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
11 dAlifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,
hema lake kumzunguka,
mawingu meusi ya mvua ya angani.
Copyright information for SwhNEN